Leo June 12, 2018 Viongozi 9 wa CHADEMA akiwemo mwenyekiti wake Freeman Mbowe wamesomewa upya mashtaka 13 ikiwemo uchochezi na kufanya mkusanyiko usio halali katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Hatua hiyo inatokana na uamuzi wa June 11,2018 ambapo mahakama iliamuru hati ya mashtaka ibadilishwe kwa sababu baadhi ya mashtaka ni batili.
Akiwasomea upya mashtaka yao Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri amedai washtakiwa wanakabiliwa na makosa 13 ambapo washtakiwa wote wapo isipokuwa Esther Matiko anayedaiwa kuumwa.
Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika.
Katibu wa chama hicho Dk.Vicenti Mashinji, mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na mbunge wa bunda, Esther Bulaya.
Miongoni mwa mashtaka hayo 13 ni kula njama, ambalo linawakabili washtakiwa wote wakidaiwa February 1 na 16, 2018, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko kutawanyika.
Pia wanadaiwa February 16,2018 katika viwanja vya Buibui na Mwananyamala Kinondoni wakiwa wamekusanyika na adhma ya pamoja, waliitekeleza kwa kufanya mkusanyiko usio halali na kusababisha watu waogope kuwa watakwenda kupelekea uvunjïfu wa aman
Pia wanadaiwa kuwa February 16,2018 katika barabara ya Kawawa Kinondoni Mkwajuni washtakiwa hao wakiwa na wenzao 12 ambao hawapo mahakamani walikiuka tamko la kuwataka kutawanyika la Afisa wa polisi SSP, Gerald Ngiichi kwa kugoma kutawanyika na kupelekea uvunjifu wa amani.
Inadaiwa kugoma huko kulipeĺekea hofu na hatimaye kusababisha kifo cha Akwilina Akwiline na majeruhi kwa askari wawili ambao ni H.7856 PC Fikiri na E.6976 CPL Rahim Msangi.
Shtaka jingine la uchochezi wa uasi linamkabili Mbowe ambapo anadaiwa February 16,2018 katika maeneo Dar es Salaam, alitoa matamshi ya kupandikiza chuki na dharau kwa upande wa raia wa Tanzania dhidi ya mamlaka halali.
Shtaka jingine linamkabili Esther Buĺaya akidaiwa February 16, 2018 katika viwanja vya Buibui wilayani Kinondoni, Dar es Salaam alïtenda kosa la kukaidi amri halaĺi ya tamko la Jeshi la Polisi.
Baada ya kusomewa makosa hayo washtakiwa waliyakana ambapo wakili Nchimbi aliomba tarehe kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali.
Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi June 18,2018.