Mpenzi wa sasa wa staa wa muziki nchini Marekani Ariana Grande amekubali ishu ya kumvalisha pete ya uchumba mwanadada huyo katika mahojiano aliyofanya na kipindi cha television ambacho ni maarufu nchini Marekani The Tonight Show.
Pete Davidson ambaye ni mchumba wa sasa wa staa huyo ameongelea furaha aliyonayo ikiwa ni miezi mitatu tu tokea wajuane na Ariana Grande na kumvalisha pete ya uchumba na kusema kuwa ni kitu ambacho hakukitegemea katika maisha yake na anahisi kama ameibuka mshindi katika mashindano.
Pete Davidson alisema kuwa “Ni kitu kizuri sana kwa sababu ukipita mtaani vijana wengi wanakupa heshima kwa kitendo hicho”
EXCLUSIVE: Aika kaeleza upekee wa style yake ya nywele na sababu kuiweka