Leo June 22, 2018 kutoka mkoani Arusha kuna hii ya kuifahamu kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo imesaini mkataba wa EURO Milioni 39, kwa kipindi cha miaka minne kwa ajili ya kuisaidia Jumuiya hiyo kwenye masoko ya Ulaya.
Akizungumza wakati wakutia saini makubaliano hayo Katibu Mkuu wa EAC, Liberat Mfumukeko amesema kupitia fedha hizo zitasaidia kuboresha bidhaa zinazozalishwa ili ziweze kumudu soko la kimataifa.