Kutokana na mujibu wa chart za Billboard nchini Marekani wimbo wa “Sad” kutoka kwa marehemu rappa Xxxtentacion umetoka rasmi leo June 28,2018 na kwenye video ya wimbo huo unamuonyesha akihudhuria mazishi yake mwenyewe.
Kupitia video ya ngoma hiyo iliyoandikwa na Marehemu Xxxtentacion na kuongozwa na James Pereira “JPM” inaonyesha baadhi ya sehemu rappa Xxxtentacion akiulizwa maswali na mtu aliyejificha kila sehemu .
Rappa Xxxtentacion kwa sasa amepumzishwa katika nyumba yake ya milele ambapo June 27,2018 familia ya marehemu iliuaga mwili wake na mashabiki wengi walijitokeza kuuaga mwili huo.
Povu la Mke wa Chege kwa wanaomfuata DM juu ya Mumewe ‘Muhuni si handsome’