Leo June 29, 2018 Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imemgundua Elia Emanuel, Mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo cha Maabara mkoani Singida kuwa ndiye kijana aliyesambaza Video ya uvumi wa kuwepo kwa dawa aina ya Panadol iliyosadikiwa kuwa baada ya kuloweshwa hugeuka kuwa taulo.
TFDA imekanusha taarifa za kuwepo kwa dawa hiyo na Mwanafunzi huyo amesema alipata video hiyo kwenye mtandao na ilikuwa kwa lugha ya Kingereza na akaitumia kama chanzo cha uhakika kwa kuitafsiri kwa Kiswahili kisha kuisambaza kitandaoni.
MAGAZETI LIVE: Biashara ya kushikwa nyeti, matiti yaibuka, Mateso ya korosho