Leo June 29, 2018 nakuletea stori kutoka huko nchini Uganda ambapo unaambiwa kuwa Maafisa wa Polisi nchini Uganda wanaripotiwa kukataa kuwalinda Wabunge wa nchini humo kwa kile wanachokidai kuwa maisha ya Wabunge hao yamo hatarini hivyo kuwalinda ni kama kujitafutia kifo.
Taarifa hizo zimefichuliwa katika mkutano kati ya Wabunge wa Uganda na Rais Museveni ambapo Wabunge hao walimweleza Rais Museveni jinsi ambavyo Polisi wa nchini humo wanavyokataa kuwapa ulinzi.
Na baada ya kuthibitishwa kwamba maafisa wa polisi wanaogopa kuwapa ulinzi Wabunge, Rais Yoweri Museveni amemwelekeza mkuu wa jeshi Generali David Muhoozi, kutoa ulinzi wa kijeshi kwa wabunge hao, na kutaka mkuu wa polisi Okoth Ochola kuwafuta kazi polisi ambao wamekataa kuwalinda wabunge.
Aidha Mbunge wa upinzani Kaps Fungaroo amesema kuwa baadhi ya Polisi wanasema kuwa ni bora wa wafutwe kazi kuliko kuwalinda Wabunge.
Kwa sauti ya Rais Magufuli “IIIIIH!! WATAPATA TABU SANA!”