Waziri wa Maliasili na Utalii Dr Hamisi Kigwangalla ametoa miezi mitatu kwa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kufanya utafiti na sensa ya mamba katika ziwa Rukwa ili kubaini idadi yake na hatimaye kuishauri Serikali namna ya kudhibiti madhara yanayosababishwa na mamba hao kwa wananchi hususani katika jimbo la Songwe na ikibidi kuwavuna kama idadi yao itabainika kuwa kubwa.
“Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori ambayo ipo chini ya Wizara yangu, nawaagiza wafike hapa mara moja na ndani ya miezi mitatu wanipe majibu nini kifanyike kupunguza madhara yanayotokana na mamba kwenye ziwa Rukwa, wafanye sensa watuambie kuna Mamba wangapi lakini pia watushauri nini tufanye ili kudhibiti mamba hao wasiendelee kusababiaha athari kubwa kwenye maisha ya watu wanaoishi jirani lakini pia wanaoutumia ziwa” –Kigwangalla
“Kwa sababu madhara yanaweza yakawa mengi, inawezekana mamba wameshakuwa wengi na samaki wamebaki wachache, kwahivyo hata mamba nao mwishowe wataanza kufa ama wataanza kutafuta chanzo kingine cha chakula pengine ndio maana wameanza kutafuta binadamu anayekwenda ziwani kwasababu sasa wanakuwa na njaa, inabidi wasogee ufukweni wawinde chochote kinachosogea karibu na maji” –Kigwangalla
Gigy Money alilimiss buku la Mo J “tunataka kuzaa mtoto wa kiume”