Leo July 2, 2018 Viongozi 9 wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti Freeman Mbowe wamemtaka Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu anayesikiliza kesi yao ajitoe kwa madai hawana imani naye.
Hakimu anayesikliza kesi hiyo Wilbard Mashauri, ambapo hadi muda huu anaendelea kusikiliza hoja kuhusu kutakiwa ajitoe.
Miongoni mwa viongozi waliotoa hoja hiyo ni Mbowe ambaye amedai ni adhabu tosha kwa upande wao kuripoti kituo cha Polisi cha kati kila Ijumaa.
“Kwa miezi 3 kila siku ya Ijumaa tunakwenda kuripoti hiyo ni adhabu tosha ukizingatia sisi ni viongozi wa umma,”amedai.
Amedai kuwa kundi lao wote ni viongozi na wanatokea sehemu mbalimbali na wanamajukumu katika maeneo wanayitokea.
Pia amedai kuwa wanakosa haki za msingi kwa sababu mawakili wao wamekuwa wakipingwa wazi wazi pindi wanapowasilisha pingamizi zao.
Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji, Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika.
Pia wengine ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya na Mbunge wa Tarime mjini, Esther Matiko.
Inadaiwa kuwa washtakiwa walitenda makosa hayo February 16, mwaka huu katika maeneo ya Viwanja vya Buibui, Mwananyamala na barabara ya Kawawa Kinondoni Mkwajuni.
Wanadaiwa kuwa Februari 16,mwaka huu katika barabara ya Kawawa Kinondoni Mkwajuni washitakiwa hao wakiwa na wenzao 12 ambao hawapo mahakamani walikiuka tamko la kuwataka kutawanyika la Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Gerald Ngiichi kwa kugoma kutawanyika na kupelekea uvunjifu wa amani.
Inadaiwa kitendo cha kugoma kulisababisha hofu iliyochangia kifo cha Mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline na majeruhi kwa askari wawili ambao ni H.7856 PC Fikiri na E.6976 CPL Rahim Msangi.
Mambo Matano yaliyosababisha JPM mabadiliko Wizara ya Mambo ya Ndani