Usiku wa July 2 2018 ulichezwa mchezo wa sita wa hatu ya 16 bora ya World Cup 2018 kati ya timu ya taifa ya Ubelgiji dhidi ya timu ya taifa ya Japan katika uwanja wa Rostov nchini Urusi yanapofanyika michuano ya World Cup 2018.
Japan ambao walipita kwa kipengele cha fair play na kuiacha Senegal ikiaga michuano hiyo, licha ya kuanza kupata magoli mawili ya mapema kupitia kwa Haraguchi dakika ya 48 na Inui dakika ya 52, mchezo ulibadilika na Ubelgiji kupindua matokeo kwa kufunga magoli matatu.
Ubelgiji walipata magoli dakika ya 69 kupitia kwa Vertonghen, dakika ya 74 kupitia kwa Fellaini na mwisho dakika nne za nyongeza Chadli akafunga goli la ushindi kwa Ubelgiji na Japan kuaga michuano hiyo kwa kipigo cha jumla ya magoli 3-2.
Baada ya game mashabiki wa Japan waliokuwepo katika uwanja wa Rostov walionesha tabia ya kushangaza kwa kuendelea na utamaduni wao wa kusafisha uwanja eneo walilokuwa wameakaa na kuliacha safi kitu ambacho ni nadra kutokea wakati wachezaji wa Japan nao wakaacha dressing room yao wameisafisha na kuacha ujumbe ulioandikwa kwa lugha ya kirusi ila una maana ya “Asante”
Haji Manara kapenda usiku wa VPL ila kafunguka wasiwasi wake