Leo July 3, 2018 Mwanamke mmoja amelazwa katika hospitali ya Leratong baada ya kukutwa hai katika jokofu kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.
Mfanyakazi katika chumba hicho aligundua bado mwanamke huyo anapumua wakati alipofika kuutizama mwili na kutayarisha nyaraka kumhusu.
Mwanamke huyo alifikishwa katika chumba hicho baada ya madaktari kusema amefariki kutokana na kutoonesha dalili zozote za uhai kufuatia ajali ya barabarani aliyoipata.
Familia ya mwanamke huyo imesema wamepata mshtuko mkubwa na wana wasiwasi kuhusu mkasa huo hivyo wanahitaji ufafanuzi ni vipi makosa hayo yanaweza kutokea.