Hii ni nyingine ya kuifahamu kutoka kwa staa Davido ambaye amezua gumzo kwenye mtandao wa Instagram baada ya kupost picha ya mpenzi wake Chioma na kuandika caption ambayo imezua maswali na wengi kujiuliza “Je Davido yupo mbioni kumuoa Chioma?”.
Kupitia ukurasa wa instagram wa Davido ameandika caption inayosema “Mpenzi wa maisha yangu, siwezi kusubiri kuwa na wewe milele” wengi wameichukulia kauli hiyo kama Davido anataka kumuoa Chioma, kwani kitu pekee kinachowafanya wapenzi waishi milele ni ndoa.
Licha ya kwamba Davido ana watoto wawili aliyozaa na wanawake wawili tofauti tofauti hii imeonekana kuwa ya toafauti kwa mpenzi wake Chioma baada ya kuamua kumuweka hadharani ili watu wamtambue na kuandika maneno yanayoashiria kuwa hakuna mwanamke mwingine mwenye nafasi kwake.
Shoe Shiner anayeingiza zaidi ya LAKI TANO, ameajiri vijana, anasomea Degree