Usiku wa jana July 15,2018 timu ya taifa ya Ufaransa kwa mara ya pili ilifanikiwa kutwaa taji lake la pili la World Cup 2018 kwa kuifunga timu ya Croatia kwa magoli 4-2 ikiwa ni baada ya miaka 20 kihistoria, katika list ya wachezaji 23 waliowakilisha taifa la Ufaransa 15 wana asili ya Afrika huku watatu wana asili ya mataifa mengine na watano ndio wana asili ya Ufaransa.
Wengi wamefurahia ubingwa huo wa Ufaransa ikiwa asilimia kubwa ya wachezaji wake wana asili ya Afrika akiwemo Rapper P Diddy ambaye ameonyesha furaha hiyo kupitia ukurasa wake instagram ambapo amepost ujumbe ulioandikwa na Khaled Beydoun kupitia twitter na kuandika
“Wapendwa Ufaransa, Hongereni kwa ushindi wa kombe la dunia, aslimia 80 ya wachezaji ni Waafrika tupilia mbali ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni, asilimia 50 ya wachezaji ni Waislamu tupilia mbali chuki dhidi ya waislam, hivyo Waislam na Waafrika wamewaletea kombe la pili la dunia sasa wapeni haki”
P Diddy aliandika caption inayosema “Mara chache huwa tuna wasiwasi sasa tuangalie mambo ambayo hayaongelewi, sisi kama watu wenye rangi nyeusi tunahisi kila kitu, sasa hivi tutalifanyia kazi, sichukulii mbali huu ushindi ni wa kihistoria, hebu tuwajali vizuri na Wamerakani wafanye hivyo”
Cristiano Ronaldo alivyowasili Turin na private jet