Rapper maarufu kutokea kwenye kundi la Maybach Music Group MMG kutokea Marekani Wale ambaye anatamba na ngoma yake kali ya “My Love” aliyowashirikisha Wizkid, Major Lazer na Dua Lipa amenusurika na ajali mbaya ya gari iliyotokea usiku wa Jumamosi July 14,2018.
Kupitia ukuarasa wake wa twitter ametoa taarifa hizo kuhusiana na ajali hiyo aliyoipata na kunusurika na pia amesema kuwa ingekuwa mbaya zaidi lakini anamshukuru Mungu kwa kila kitu kutokana na yeye kuwa kwenye kiti cha nyuma ya gari.
Rappa huyo ametamba na ngoma nyingi kali ikiwemo na kutoa album ya Ambition 2011, The Gifted 2013,shine 2017 na nyingine nyingi na kwa sasa yupo ukingoni kudondosha Album yake mpya hivi karibuni.
‘Ushindi wa Ufaransa ni wakihistoria, tuache ubaguzi’- P Diddy