Bado mambo sio mazuri ndani ya club ya Yanga kwani licha ya kushindwa kukamilisha usajili wa wachezaji watatu akiwemo Deus Kaseke kwenda CAF kwa ajili ya kumtumia katika michuano ya Kombe la shirikisho Afrika,
Leo July 18 2018 zimeanza kuenea tetesi katika mitandao ya kijamii kuhusiana na Katibu Mkuu wa Yanga Boniface Mkwasa kuandika barua ya kujiuzulu kimyakimya, kwa madai licha ya kujitoa kwa hali na mali lakini kuna watua wanamkwamisha.
Hivyo kwa mujibu wa muandishi wa habari za michezo Shaffih Dauda zimeripotiwa tetesi hizo huku wengine, wakidaiwa kupanga namna ya kumbembeleza Mkwasa kufuta uamuzi huo, AyoTV na millardayo.com zinafuatilia kwa kina tetesi hizo ili kujua ukweli kutoka vyanzo husika.
Cristiano Ronaldo alivyowasili Turin na private jet