Staa wa club ya Arsenal na timu ya taifa ya Ujerumani Mesut Ozil usiku wa July 22 2018 amefikia maamuzi mazito ya kutangaza kustaafu kucheza timu ya taifa ya Ujerumani.
Ozil kupitia barua yake aliyoisambaza katika mitandao ya kijamii, amefikia maamuzi ya kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani ameeleza kuwa amestaafu baada ya kudai kuwa anabaguliwa kutokana na asili yake kuwa Uturuki.
Hata hivyo wanasiasa Ujerumani wamewahi kumtuhumu kwa kumuita Ozil msaliti baada ya kupiga picha na Rais wa Uturuki Erdogan na amewatuhumu viongozi wa chama cha soka Ujerumani DFB kwa kutomuheshimu.
Ozil anafikia maamuzi hayo ya kustaafu akiwa na umri wa miaka 29 na ameichezea timu ya taifa ya Ujerumani jumla ya game 92, akifunga magoli 23 na assist 33 akiisaidia Ujerumani kutwaa World Cup 2014 nchini Brazil, Ozil amewahi kutangazwa mchezaji bora wa Ujerumani DFB mara tano.
USAJILI WA YONDANI: Manara asema “Mimi ndio msemaji wa SIMBA SC”