Leo August 1, 2018 Watoto mapacha walioungana sehemu ya kifua na tumbo ambao walizaliwa katika Hospitali ya Sekou Toure wamefariki leo saa 11 alfajiri wakiwa wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Bugando.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Lucy Mgole kwa niaba ya Mkurugenzi wa Bugando imesema kuanzia jana hali ya Upumuaji ya watoto hao mapacha ilibadilika na kuwa mbaya licha ya kupata msaada wa kupumua wa hewa Oxgen toka kwenye mashine.