Mtendaji mkuu wa club ya Bayern Munich ya Ujerumani Karl-Heinz Rummenigge leo amechukua headlines baada ya kutoa mawazo yake kuhusu usajili wa Cristiano Ronaldo wa euro milioni 100 kutoka Real Madrid kwenda Juventus akiwa na umri wa miaka 33.
Mabingwa wa Italia Juventus mwezi uliopita walimsajili Ronaldo kwa rekodi ya uhamisho wa dunia kuwahi kufanya kwa wachezaji wanaocheza Italia, uhamisho wa Ronaldo umechukua headlines kutokana na umri wake, wengi wanaamini mchezaji aliyepaswa kununuliwa kwa dau hilo chini ya miaka 30.
“Ronaldo? nimeshangazwa na Andrea Agnelli kumsajili Ronaldo kwenda Juventus lakini kwa mtazamo wa Juve ina maana flani hivi, maana soka la Italia kwa miaka ya hivi karibuni limepoteza mvuto lakini kwa upande wetu sisi tusingeweza kuwekeza pesa zote kwa mchezaji mwenye miaka 33” >>> Karl-Heinz Rummenigge
Karl-Heinz amemshangaa maamuzi ya mwenyekiti wa Juventus Andrea Agnelli kufanya usajili wa Ronaldo kwa pesa zote hizo, hadi sasa Bayern Munich wametumia kiasi cha pound milioni 17 kwa kumsajili Alphonso Davies mwenye miaka kutokea club ya Vancouver ya Canada.
“Nimeenda chumbani kwa Canavaro, alichonijibu SINTOSAHAU”-Edo Kumwembe