Moja kati ya wachezaji hatari katika suala la kushambulia na kufumania nyavu ni mshambuliaji wa zamani wa club ya Man United Zlatan Ibrahimovic anayeichezea club ya LA Galaxy ya Marekani kwa sasa.
Mashabiki wa soka wengi waliamini kutokana na Zlatan kuwa na umri wa miaka 35 wakati akipata majeraha ya goti akiwa na Man United itakuwa ngumu kurudi uwanjani akiwa bora, Zlatan July 29 2018 amefunga hat-trick yake ya kwanza MLS akiwa na LA Galaxy katika mchezo dhidi ya Orlando City uliyomalizika kwa LA Galaxy kupata ushindi wa magoli 4-3.
Baada ya ushindi na kufunga hat-trick yake ya kwanza Zlatan, leo kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika ujumbe mfupi akiashiria kuwa yeye bado yupo sawa licha ya kuwahi kuambiwa ameisha, Zlatan leo amepost picha ya jeraha lake la goti katika instagram account yake na kuandika “Walisema nimekwisha, niliwaambia hapana”
“Nimeenda chumbani kwa Canavaro, alichonijibu SINTOSAHAU”-Edo Kumwembe