Jioni ya leo August 4, 2018 Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameungana na viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, kumpokea Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala ambaye amesafirishwa kwa ndege kutoka Arusha alikopata ajali leo asubuhi, kuja DSM kwa matibabu zaidi.
Dkt. Kigwangalla amepata ajali leo majira ya saa 12:15 asubuhi katikati ya vijiji vya Mdolii na Minjingu Wilaya ya Babati Mkoani Manyara baada ya gari lake kupinduka na kusababisha kifo cha Afisa Habari wa Wizara ya Maliasili na Utalii Hamza Temba na wengine watano akiwemo Dkt. Kigwangalla kuumia.
Baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini DSM, Dkt. Kigwangalla amepelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu.
Katika mapokezi hayo Rais Magufuli alikuwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (aliyemsindikiza Dkt. Kigwangalla), Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Maliasili Mej Jen. Gaudence Milanzi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya.
Akizungumza Rais Magufuli amempa pole Dkt. Kigwangalla na kumuombea apone haraka na pia amewashukuru madaktari na wauguzi wa Kituo cha afya cha Magugu walioanza kutoa huduma ya kwanza na amewashukuru Madaktari na wauguzi wa hospitali ya Selian iliyopo Mjini Arusha kwa juhudi kubwa walizofanya kuokoa maisha ya Dkt. Kigwangalla na majeruhi wengine wa ajali hiyo.
Mbunge Lema anatueleza hali ya Kingwangalla baada ya kumtembelea hospitalini
TOP 8: MATUKIO MAKUBWA YA KUKUMBUKWA UAPISHWAJI WA MHESHIMIWA JOKATE