Leo August 13, 2018 Katibu Mkuu wa CCM, Dr. Bashiru Ally, amesema amempa maagizo Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ampe maelezo kwa nini polisi wanawanyanyasa waendesha bodaboda, ikiwa ni pamoja na kuwalipisha ushuru tofauti na ulioandikwa kwenye leseni na kwa nini wanawakamata hata kama hawana makosa.
Dr. Bashiru ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho zilizopo Lumumba DSM, ambapo mbali na mambo mengine, amempokea aliyekuwa Mbunge wa Liwale kwa tiketi ya CUF, Zuberi Kuchauka aliyerejea CCM.
“Nchi yetu kwa kiwango kikubwa bado kuna amani, yako matukio ambayo lazima tusimamie yasitokee, Kakonko nimeambiwa kuna Askari anafunga watuhumiwa kwenye miti nimeagiza atafutwe, nimemwambia Waziri Lugola anieleze kwa nini stika ya elfu moja iandikwe elfu mbili” Bashiru
Katibu Mkuu CCM “Monduli mashambulizi yake lazima yawe usiku, vita ni muda wote”