Baada ya the female Rapper Nicki Minaj kudondosha ya moyoni katika mahojiano aliyoyafanya na kipindi cha radio cha Hot 97 na mtangazaji Dj Funkmaster Flex na kumzungumzia vibaya mpenzi wake wa zamani Safaree Samuel.
Nicki Minaj alifunguka na kusema alikuwa akimuhudumia kila kitu mpenzi wake hadi ilifikia muda Safaree alikua akiiba kadi yake ya benki na kuchukua hela na kuzitumia hela hizo kununua wanawake pia Nicki Minaj alikanusha kuhusiana na taarifa zinazosambaa kuwa alikuwa akiandikiwa ngoma kadhaa na Safaree.
Inaonekana muendelezo wa vita umeendelea katika mtandao wa twitter ambapo Safaree amefunguka mengi tusiyoyajua kuhusiana na Nicki Minaj na kusema kuwa aliwahi kuchomwa kisu na Nicki Minaj kitu ambacho kilihatarisha maisha yake ila baada ya polisi kufika eneo la tukio alisema kuwa amejichoma mwenyewe ili kumnusuru mpenzi wake asiende jela.
Safaree ameendelea kwa kusema kuwa sasa hivi Nicki Minaj anatakiwa kupromote Album yake mpya na sio anapoelekea na ana amini kuwa kwa level aliyoifikia hatakiwi kufanya vitu kama hivyo.
Steve kafunguka kununua Shamba la Mzee Majuto “Mimi ni paka, sifi kizembe”