Taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii jioni hii ni kuhusiana na kifo cha muimbaji, mtunzi wa nyimbo na mpigaji piano kutokea nchini Marekani Aretha Franklin ambaye alifahamika kama “Malkia wa Soul” ambaye amefariki leo August 16,2018 akiwa na umri wa miaka 76.
Aretha Franklin alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa saratani kwa muda mrefu na kulazwa hospitalini siku kadhaa zilizopita, huku ndugu zake wa karibu walipewa taarifa na madaktari kuwa alibakiza siku chache tu za kuishi duniani kutokana na ugonjwa huo kufikia hatua ya mwisho.
Marehemu Aretha Franklin alitamba na hits kali enzi za uhai wake kama Natural woman, Chain of Fools, Freeway of Love na nyingine nyingi, mwaka 1991 alishinda tuzo tatu kutokana na mchango mkubwa aliounyesha katika music industry huku akiwa na jumla ya tuzo 20 za Grammy.
MAMA HAMISA: “Hamissa amelipwa hela ndefu, mimi ni meneja wake”