Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola amemuagiza Mkurugenzi wa makosa ya jinai nchini DCI kumkamata aliyekuwa Mkurugenzi wa NIDA Dickson Maimu pamoja na watumishi wengine wa NIDA waliohusika katika tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma na kisha kuwapeleka katika Mahakama ya mafisadi.
Lakini pia Waziri Lugola ameamuru kukamatwa kwa wadhabuni watatu walioshindwa kurejesha fedha wanazodaiwa na Serikali ambapo nao wataunganishwa katika Mahakama hiyo ya mafisadi.