Baada ya msanii na Mbunge Bobi Wine kukamatwa kwa tuhuma za kudaiwa kuiponda serikali ya Uganda iliyopo chini ya Rais Yoweri Museven mdogo wa superstaa Chameleon, Pallaso ameamua kuachia ngoma ambayo inataka mbunge huyo aachiwe huru.
Pallaso ambaye pia ni msanii kutokea uganda aliachia ngoma ya “Free Bobi Wine” August 20,2018 kwa dhumuni la kufikisha ujumbe kwa jamii ili waungane katika kumsaidia Bobi Wine apate uhuru akiamini kuwa Bobi Wine anafanya hivyo ili kuwasaidia wananchi wa Uganda.
Katika mahojiano ya simu aliyofanya Pallaso na site ya Uganda ya Howwe amesema kuwa “Nimeandika huu wimbo kwasababu nahisi tunahitaji amani na pia najaribu kupeleka ujumbe kwa jamii kulingana na ninavyojiskia na ninachoskia kwa watu. Bobi Wine sio mume tu bali ni baba na pia ni mtoto kwa Taifa, yeye ni alama ya matumaini kwa vijana wengi”
“Tunamatumaini na kuamini kuwa anachokisamamia sio kuipinga serikali bali ni kuleta kile kinachohitajika zaidi katika nchi ya Uganda”
B- DOZEN KAFUNGUKA: NDOA YA KIMYA KIMYA NA BOSS WAKE,