Kwa mujibu wa mtandao wa The Blast umeripoti kuwa mzazi mwenza na Chris Brown, anayejulikana kwa jina la Nia Guzman amefungua kesi Mahakamani akidai kuongezewa hela ya matumizi ya mtoto wao Royalty mwenye umri wa miaka minne.
Nia Guzman amefungua mashtaka hayo akiwa chini ya Mwanasheria Lisa Bloom na kudai kuwa pato la Chris Brown limeongezeka kwa miaka miwili iliyopita ambapo linatajwa kufikia dola za Kimarekani 350,000 sawa na zaidi ya Tshs Millioni 800.
Nia Guzman ameiambia Mahakama ya California kuwa Chris Brown anamlipa kiasi cha zaidi ya Tshs Millioni 5 kwa mwezi hivyo kutokana na mapato yake kuongezeka anastahili kupokea Tshs Millioni 48. Nia Guzman amesema kuwa anapata kipato cha shillingi laki 9 kwa mwezi kutoka kwenye duka la nguo la mtoto wake Royalty lililopo mtandaoni.
Hii sio mara ya kwanza kwa wawili hawa kuingia kwenye mgogoro na kupelekana Mahakamani juu ya matumizi ya mtoto, ikiwa mwaka 2017 Nia Guzman alifungua mashtaka lakini baadae yalitupiliwa mbali.
Gigy Money karudi tena, time hii ni Zari ‘Bora nikate mauno lana’