Mtandao wa TMZ unaripoti kuwa Colin Kaepernick ambaye kwa sasa ni mchezaji huru amewafurahisha wengi baada ya sura yake kutumiwa na kampuni ya Nike huku akisaini dili nono kwenye kampeni ya “Just Do It” kuelekea sherehe za kuadhimisha miaka 30 kampuni hiyo.
Dili hilo linamfanya Colin Kaepernick kutangaza mavazi pamoja na bidhaa nyingine za kampuni hiyo ambapo alianza kushirikiana na kampuni hiyo ya Nike mwaka 2011 huku wengine waliotajwa kushiriki kwenye kampeni hiyo ni Serena Williams, Odell Beckham, Lebron James.
Jamii ya watu weusi “Black Americans” wamefurahishwa na kitendo hicho ikiwa Collin alipata umaarufu mkubwa baada ya harakati zake za kuanza kupiga goti moja wakati wa kuimba wimbo wa Taifa kwenye kila mchezo wa ligi ya NFL kutokana na kauli za ubaguzi wa rangi za Rais Donald Trump.
Mchezaji huyo wa zamani wa soka la Marekani aliyekuwa akiichezea timu ya San Francisco 49ers inasemekana kuwa kwa sasa hana timu yeyote tokea mwaka 2016 na kupitia ukurasa wake wa twitter aliandika “Amin katika kitu flani hata ikibidi kutoa sadaka kila kitu” baada ya kupewa dili na kampuni ya Nike.
Madee kuhusu Dogo Janja na Irene Uwoya “HAIPITI WIKI LAZIMA?”