Cardi B pamoja na Nicki Minaj nusu wazichape usiku wa September 7,2018 kwenye sherehe ya Harper’s Bazaar Icons Party ambayo ni sherehe maalum kwenye wiki ya maonyesho ya mitindo Marekani “New York Fashion Week”.
Inaripotiwa kuwa Cardi B aliwasili wa kwanza kwenye sherehe hiyo na baadae Nicki Minaj alifata lakini baada ya kuwasili kwa Nicki Minaj ugomvi ulianza huku wakiwa wanarushiana maneno makali na kutaka kupigana lakini watu waliwazuia kwa kuwashika.
Wawili hao wanadaiwa kuwa kwenye beef kwa kipindi kirefu lakini safari hii kila mtu ameonekana kuonyesha hisia zilizokuwa zikijificha ndani yao, Cardi B alionekana kupata jeraha usoni na kulazimika kuondoka mapema kwenye sherehe hiyo kutokana na nguo yake kuchanika.
Kutokana na video zinazosambaa zinaonyesha Cardi B akisikika akilalamika kuhusu mtu kumsema mtoto wake Kulture lakini bado haijajulikana chanzo cha ugomvi huo mpaka kufikia hatua ya kurushiana viatu.
Kupitia ukurasa wa instagram wa Cardi B ameandika ujumbe huu “Nimeacha vingi vipite,nimekuacha uniseme na kudanganya kuhusu mimi umenizibia riziki zangu lakini nakula, umewatishia wasanii kwenye muziki na kuwaambia wakifanya kazi na mimi hutokuwa nao karibu”
“Nimekuacha uongelee vingi kuhusu mimi, nilikufata mara moja binafsi na nikakufata tena kwa mara ya pili, lakini ukimtaja mwananngu unachagua kupenda maoni kuhusu mimi kama mama, nimefanya kazi kwa bidii na nimetoka mbali kwahiyo sitoruhusu mtu acheze na mafanikio yangu”
“Mnaongea sana na kurap laikini kwa maisha ya uhalisia hampo mlivyo, kweli kila kitu ni kwaajili ya burudani”
https://youtu.be/UWjrzxpUOh8
CALISAH asitisha huduma ya kampuni yake ya mbegu za kiume