Tupilia mbali sakata la kutaka kupigana na Nick Minaj, time hii Cardi B amewashangaza wengi baada ya kushirikiana na kampuni ya urembo nchini Marekani Tom Ford Beauty kwa kupiga dili la lipstick zenye jina lake.
Kupitia ukurasa wa instagram wa Cardi B ameishukuru kampuni hiyo ya Tom Ford kwa kushirikiana naye na kusema kuwa ana shauku ya kuendelea kufanya nao kazi na kuzindua vitu vingi mbeleni.
Lipsticks hizo zenye jina la Cardi B zimeonekana kuuzika haraka kwa muda mfupi, hii ni baada ya toleo la kwanza kuwekwa sokoni na mauzo yake kuonekana kuwa juu zaidi kuliko matarajio ndani ya muda mfupi, kitu ambacho kimewafurahisha wengi akiwemo Cardi B mwenyewe.
Lulu amemaliza kimya chake cha siku 323 leo