Ikiwa ni miaka 17 imepita tangu kutokea kwa shambulio kubwa la kigaidi Marekani ambalo kamwe halitosahaulika ,tukio hilo la kigaidi liliyakumba majengo mawili yanayotizamana yajulikanayo kama “Twin Towers” yenye jumla ya ghorofa 220 katika mji wa New York siku ya Jumanne September 11,2001 .
Nchi ya Marekani inaikumbuka siku hii kwani iligharimu maisha ya watu takribani 3000 na kujeruhi vibaya watu zaidi ya elfu 6 na kusababisha hasara katika nchi ya Marekani sawa na Dolla billion kumi ambazo ni zaidi ya Trillion 22 za Kitanzania,
Jeshi la Polisi la Marekani lilitoa taarifa kuwa askari 78 walipotea katika tukio hilo na kusadikiwa kuwa miili yao haikuonekana na takribani wafanyakazi wa kikosi cha zima moto 200 walifariki kutokana na kujaribu kuokoa watu.
Inasemekana shambulio hilo lilifanywa na kundi la kigaidi lijulikanalo kama Al-Qaeda lililokuwa likiongozwa na mshukiwa namba moja Osama bin Laden ambapo inasemekana kuwa aliteka nyala ndege nne na wakazitumia kama silaha na kugongesha ndege hizo katika majengo ya New York, Pentagon na Washington DC kwa makusudi.
“Nilikuwa navunjwa moyo na Salama, Nilipambana Kumfurahisha” – Walter Chilambo