Mwanzilishi wa timu ya Tukuyu Stars iliyowahi kushiriki ligi kuu Tanzania bara miaka ya 80+ Ramnik Patel maarufu kwa jina la KAKA amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya akipatiwa matibabu baada ya kuvunjika mguu akiwa nyumbani kwake maeneo ya Uhindini jijini Mbeya.
Akizungumza anaeleza kuwa amelala hospitalini hapo kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.
Katika historia anakumbuka timu yake kuchukua ubingwa wa ligi kuu bara mwaka 1986 na kushuka daraja mwaka uliofuata. Hata hivyo hakukata tamaa bali aliendelea na kisha kuirejesha tena ligi kuu mwaka 1988.
Kwa sasa anauguzwa na familia yake ambayo inagharamia gharama zote za matibabu Mkewe Neva Patel na mwanae wa mwisho Hinnabery ndio wameshikiria jukumu hili.
Kulingana na daktari wa mifupa Josephati Kamugisha anayemtibu KAKA anaeleza kuwa itamchukua zaidi mwaka mmoja kupona kabisa. Hii ni kutokana kuvunjika mfupa wa nyonga kwenye mguu wake wa kushoto.
Pamoja na kuandamwa na maradhi KAKA hajasahau kuwataja baadhi ya wachezaji waliopitia mikononi mwake akiwemo Ali Kimwaga, Daniel Chundu, Kelvin Haule, Geoffrey Katepa, Sekilojo Chambua na Seleman Mrisho.
Mgambo wambeba dada Mjamzito wakimlazimisha ajiunge nao, 30 wahama Kijiji