Superstar Tiwa Savage amedai kuwa aliachwa hotelini bila kulipwa gharama za malazi alipokuwa nchini Kenya kwenye uzinduzi wa album ya mkali wa dancehall Redsan uliofanyika Jumapili September 16,2018.
Inaripotiwa kuwa Tiwa Savage alijaribu kufanya mawasiliano kwa kumpigia simu promota aliyekuwa amemualika nchini humo lakini mwisho wa siku hakukuwa na mafanikio yoyote.
Superstar huyo ambaye aliwasili Kenya Jumamosi September 15,2018 ameelezea kuhusiana na utapeli huo kupitia ukurasa wake wa twitter na kusema kuwa hakukuwa na malipo yoyote yaliofanywa hotelini na kuwataka mapromota kuacha kuwasema vibaya wasanii.
Tiwa Savage >>>“Malipo ya hotelini yote hayajafanyika, hakuna gari la kutupeleka uwanja wa ndege alafu iweje mapromota watake kuwaongelea vibaya wasanii”
NOMA! Bondia Mwakinyo alivyobebwa mgongoni na Mama yake