Fahamu vitu kadhaa alivyoviongea Nandy leo September 17,2018 kwenye mahojiano na kituo cha radio cha Clouds FM kwenye kipindi Cha Leo Tena alipoenda kutambulisha ngoma yake mpya ya “Aibu”
Nandy ameongea vitu vingi ikiwa na kuwajulisha mashabiki kuwa ifikapo 2020 ataacha rasmi muziki na kujikita zaidi kwenye biashara.
“Nina kipaji cha kuimba na hii ndio platform yangu ya kunifanya mimi niwe mfanyabiashara mkubwa, niliwaza nikipata management nzuri itanitengenezea jina”
“Malengo yangu ni kuwa mfanyabiashara mkubwa sana na hata wakati naanza kufanya muziki nilijiwekea malengo baada ya miaka mitano niache muziki na niendeleze biashara zangu”
“Mpaka sasa nimetumia miaka miwili na mwaka 2020 ndio nitaacha muziki na sio kwamba nitakuwa sitoi ngoma hapana nitakuwa natoa sema kwa mwaka hata mara moja na show naweza kuwa nafanya mara moja kwa mwaka ili nipate muda mzuri wa kusimamia biashara zangu”
“Napenda kuongea na wateja na kupunguziana ile lugha ya biashara ndio inanivutia na ndio kitu nachokipenda kukifanya”.
NOMA! Bondia Mwakinyo alivyobebwa mgongoni na Mama yake