Baada ya kushindwa kupata matokeo chanya katika michezo yake ya Ndanda FC mkoani Mtwara na Mbao FC jijini Mwanza, club ya wekundu wa Msimbazi Simba SC leo walikuwa Shinyanga katika uwanja wa CCM Kambarage kucheza mchezo wao tatu ugenini dhidi ya Mwadui FC.
Simba wakiwa Shinyanga baada ya kupoteza jumla ya point tano katika michezo ya Ndanda na Mbao FC, leo walirekebisha makosa na kuifunga Mwadui FC kwa magoli 3-1, magoli ya Simba SC yakifungwa na nahodha wao John Bocco dakika ya 41 kwa penati na dakika ya 45 kabla ya kwenda mapumziko.
Kipindi cha pili baada ya kuanza Simba wakapata goli la tatu dakika ya 51 kupitia kwa Meddie Kagere, Mwadui iliwalazimu kusubiri hadi dakika ya 82 ili kupata goli la kufutia machozi kupitia kwa Charles Ilanfya.
Magoli mawili aliyoyafunga John Bocco yanamfanya kufunga jumla ya magoli 100 katika maisha yake ya Ligi Kuu Tanzania bara toka alipoanza kucheza 2008 akiwa na Azam FC ila Simba imepata pigo kwani itamkosa Bocco game dhidi ya Yanga kutokana na kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumpiga kichwani mchezaji wa Mwadui.
EXCLUSIVE: Licha ya kuwa na pesa na ustaa, hii ndio Sababu inayomfanya Samatta asiringe