Hii ndio kauli ya kwanza ya Maua Sama tokea aachiwe huru kwa dhamana baada ya siku kadhaa kupita tokea akamatwe na jeshi la Polisi na kufunguliwa kesi ya kwenda kinyume na sheria ya Benki Kuu kwa kudaiwa kuidhalilisha noti ya Tsh elfu 10.
Mastaa mbalimbali walitumia kurasa zao za instagram kumuombea Maua Sama atoke mapema ili aendelee na majukumu yake ya kawaida lakini leo September 27,2018 Maua Sama ametoa kauli yake ya kwanza kupitia ukurasa wake wa twitter.
“Changamoto ni njia ya kutukuza na kutuongezea ufahamu wa mengine tusioyajua ni ngumu sana kusahau niliyopitia siki 10 zilizoisha juzi zilikua ni siku ngumu zaidi katika maisha yangu ila pamoja na yote nawashukuru sana kwa mchango wenu kila mmoja kwa nafasi yake. Asanteni”
HUWEZI ACHA KUCHEKA!! MC PILIPILI AKIIMBA