Shirikisho la soka Tanzania TFF leo limetangaza rasmi mapato yaliopatikana katika mechi ya watani wa jadi kati ya Simba SC na Yanga, mchezo huo namba 72 wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara(TPL) kati ya Simba na Yanga ulichezwa Jumapili September 30 2018 Uwanja wa Taifa.
Mchezo huo ulioanza saa 11 jioni umeingiza jumla ya Watazamaji 50,168 na umefanikiwa kuingiza jumla ya shilingi milioni 404,549,000 za kitanzania, mgawanyo wa mapato hayo ni kwenye upande wa VAT ,Selcom, TFF, Uwanja, TPLB, gharama za mchezo, BMT na DRFA.
Katika fedha hizo VAT ambayo ni asilimia 18 ni shilingi milioni 61,710,864.41, Selcom milioni 17,901,293.25, TFF milioni 16,246,842.12, Uwanja milioni 48,740,526.35 huku wenyeji Simba SC wakipata milioni 194,962,105.41, TPLB milioni 29,244,315.81, gharama ya mchezo 22,745,578.96, BMT milioni 3,249,368.42 na DRFA milioni 9,748,105.27.
“Simba tumewaachia, sisi hatuna presha”-Kocha wa Yanga