Rapper Nicki Minaj ametudokezea ujio wa makala yake ya “Queen Documentary” ambayo itagusia maisha yake ikiwemo unyanyasaji aliowahi kuhushuhudia kutoka kwa baba yake mzazi na kuapa kuwa hatokubali kunyanyaswa na mwanaume.
Kwenye mahojiano aliyoyafanya Rapper huyo na Mtangazaji Lauren JNel amesema kuwa kitu kikubwa ambacho kimemuathiri hadi leo ni unyanyasaji aliowahi kuushuhudia kutoka kwa Baba yake mzazi kumpiga Mama yake hadi kufikia hatua ya kuingilia kati ugomvi wao.
Nicki Minaj ameongezea na kusema kuwa aliwahi kutojiamini tena kwa sababu tu ya Mtu mmoja ambaye alitaka kumshusha chini kutokana na unyanyasaji alioupata hadi kumpelekea kushindwa kuingia studio kuendelea kufanya kazi zake za muziki.
“Mama yangu alikubali kumuachia Baba yangu amfanyie fujo na nilikua nikiamua ugomvi wao lakini tokea hapo niliapa kuwa hakuna Mwanaume ambaye ataninyanyasa au kunifanyia fujo”
“Ilifikia wakati sikujitambua tena kwa sababu ya Mtu mmoja ambaye alinifanya nijiskie niko chini, niliogopa hadi kwenda studio mara ghafla nilipokuwa Miami nilipata mzuka baada tu ya kubadilisha mazingira na nikarudi studio za New York” –Nicki Minaj
https://youtu.be/gcaMK6MdYZY
Duh!! Spidi ya gari yamgharimu Quick Rocka