Samaki mkubwa aina ya chongoe mwenye uzito wa tani kumi ameonekana katika Bahari ya Hindi kata ya Moa wilayani Mkinga mkoani Tanga ambapo wavuvi wa eneo hilo waliweza kumvuta hadi kufika nchi kavu.
Kwa mujibu wa diwani wa kata hiyo Tua Mdingo amesema samaki huyo ni kati ya samaki adimu kuonekana na hivyo wako hatarini kutoweka katika mazingira ya bahari.
Kutokana na umuhimu wa kiumbe huyo kutakiwa aendelee kuishi wataalam waliamuru wavuvi hao kumrejesha baharini baada ya kukaa nchi kavu kwa muda wa siku mbili suala ambalo limempelekea kupungua nguvu na kusababisha kukosa uwezo wa kwenda kwenye kina kirefu cha maji.