Rapper Drake kutokea Canada ameweka wazi hisia zake za mapenzi juu ya mwanadada Rihanna na kusema kuwa aliwahi kutamani kuanzisha familia na Rihanna.
Kwenye mahojiano ya HBO aliyoyafanya Drake katika kipindi cha Lebron James amefunguka kuhusiana na hilo na kusema kuwa maisha yana mfumo wake na yana mafunzo yake na aliishia kwenye mawazo ambayo hakuyategemea.
“Kama maisha yanakupa mfumo na mafunzo mawazo yangu yaliishia kwenye ndoto na pengine ingekuwa Oh Drake ameanzisha familia na Rihanna na hiki ni kitu kizuri na kinapendezea kwenye magazeti, japokuwa nilitaka hicho kwa wakati mmoja” >>>Drake
Katika tuzo za MTV Video Music Awards 2016 Drake alifunguka kwenye stage na kusema kuwa alimfahamu Rihanna mwaka 2005 ambapo walikutana katika mgahawa mmoja mjini Toronto na alimpenda tokea akiwa na umri wa miaka 22.
VUNJA MBAVU: Mvuta bangi na bomba la maji/ Waandishi na ngamia/ Dogo chizi