“Mkataa kwao ni mtumwa” ni rapper Cardi B kwenye headlines ambaye amekataa kuwa mtumwa na hivyo kupakumbuka kwao Brooklyn na kuamua kuwasaidia watu wasiojiweza kwa kuwapatia majaketi na viatu.
Rapper Cardi B ni mzaliwa wa Brooklyn New York na amefanya tukio hilo siku ya Alhamisi October 18,2018 na kupata muitikio wa maelfu ya watu wanaoishi kwenye makazi ya umma ya Marlboro, Gravesend mjini Brooklyn .
“Lazima tuweke mifano kwa watoto muda mwingine watu wanafikiri kwamba tunafanya tu mambo yasiyofaa lakini una muda tunapaswa kuwajali watoto,jamii na kila kitu” >>>Cardi B
Elizabeth Michael ‘Lulu’ amerudi kazini