Watu watano wameripotiwa kupoteza maisha kwenye ajali ya gari iliyotokea eneo la Njirii wilayani Manyoni mkoani Singida leo October 21, 2018.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Kamshina msaidizi wa Polisi Sweetbert Njewike, amesema kuwa ajali hiyo imehusisha magari mawili ikiwemo gari dogo mali ya Wizara ya Kilimo na Chakula iliyokuwa na watu watano pamoja na lori.
Kamanda Njewike amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari ndogo iliyokuwa katika mwendokasi ikijaribu kupishana na lori.
“Gari ndogo mali ya Wizara ya Kilimo na Chakula ilikuwa ikitokea Dodoma kwenda Shinyanga ikiwa na watumishi wa wizara hiyo, ilikuwa katika mwendokasi na kugongana uso uso na Lori“, amesema Kamanda Njewike.
Amesema wakati dereva wa wizara ya kilimo akiwa kwenye harakati zake za kutaka kuyapita malori hayo, ghafla akakutana na lori lingine lenye namba za usajili RAC 152 Y mali ya Mount Meru Millers lililokuwa linatoka Kigali kwenda DSM na kugongana nalo uso kwa uso.
Kamanda Njewike amefafanua kuwa, ajali hiyo imesababisha vifo vya watumishi wote watano wa Wizara ya Kilimo waliokuwa kwenye gari yao, ambapo miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya Wilaya ya Manyoni ikisubiri kutambuliwa na kuchukuliwa na ndugu zao kwa ajili ya mazishi.
Waziri Jafo kawa surprise shule ya Ngaza “Watakula kuku mia moja”