Leo October 31, 2018 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amenusurika kupata ajali wilayani Gairo, Mkoani Morogoro baada ya basi la Hekima za Mungu kuovateki katika kona wakati gari la waziri huyo likiwa eneo sahihi.
Tukio hilo lilitokea saa 6:04 mchana wakati Waziri huyo alipokua anatokea Mjini Dodoma kuelekea DSM, katika eneo la nje kidogo ya Mji wa Gairo, basi hilo likiwa mwendokasi likiovateki katika kona, ndipo dereva wa gari la Waziri Lugola alipunguza spidi ili kuiepuka ajali hiyo.
Hata hivyo Basi hilo lilipopita, Waziri huyo aliekeza gari hilo lifuate kwa nyuma mpaka walikamate, hata hivyo Basi hilo lilikamatwa na dereva wa basi hilo kukaguliwa kama alikua na sifa ya kua dereva.
Mara baada ya kumkagua dereva huyo, Waziri Lugola alizungumza na abiria wa basi hilo lenye namba za usajili T140 AZZ ambalo lilikua linatoka DSM kuelekea Mjini Kahama mkoani Shinyanga.
“Kwanini mnashindwa kukemea hii tabia ya huyu dereva, mnataka awaue?, alitaka kusababisha ajali mbaya sana hapa, nanyi mmekaa kimya, mnafanya makosa kutokuripoti hii tabia mbaya kabisa,” Lugola.
Licha ya Dereva wa Basi hilo, Isaac Vian alikiri kosa hilo na kuomba msamaha lakini Waziri Lugola aliekeza akamatwe lakini atakapofika mwisho wa safari.