Leo November 1, 2018 Msanii wa Filamu, Wema Sepetu amesomewa kosa moja la kuchapisha video yake ya picha ya ngono kupitia ukurasa wake ya Instagram katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wema amesomewa kosa hilo na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde.
Mahakama ya Kisutu imetoa masharti ya dhamana kwa kumpiga marufuku Wema Sepetu kuchapisha/kuweka picha ama maneno ya Kingono katika ukurasa wake wa Instagramu pamoja na kusaini Bondi ya Sh.Mil 10.
BREAKING NEWS: Wema Sepetu afikishwa Mahakamani Kisutu