Hii ni kwa mashabiki wa soka duniani kote hakuna raha kama kuona timu mbili kubwa zikivaana Uso kwa Uso tena zikiwa na mashabiki lukuki, Miongoni mwa mechi za kusisimua sana katika Ulimwengu wa soka ni ile ya watani wa jadi nchini Ujerumani, miamba wa jiji la Dortmund na wababe wa jiji la Munich. Borussia Dortmund vs Bayern Munich na Der Klassiker ndio jina halali la mchezo huo.
Dortmund ambao wanaongoza Ligi watakuwa nyumbani katika dimba la Signal Iduna Park Jumamosi ya November 10, saa 20:30 saa za Afrika Mashariki, kuwakabili mabingwa watetezi wa ligi hiyo msimu uliopita FC Bayern Munich.
Mpaka sasa Dortmund hawajapoteza mchezo wowote katika Bundesliga msimu huu huku Bayern wao wakiwa wameshapoteza michezo miwili hadi sasa. Dortmund waliambulia vipigo katika mechi tatu zilizopita za Der Klassiker, lakini wikendi hii wanayo nafasi ya kubadili hali ya hewa, kwani wanacheza kandanda safi msimu huu huku wapinzani wakionesha kutokuwepo katika kiwango kilichozoeleka kwa miaka kadhaa sasa.
Mchezo wa Dortmund na Bayern Munich unaojulikana kwa jina la Der Klassiker pia kwa Ujerumani unajulikana kwa jina jinginge la ‘German Clasico’, je Dortmund hiyo ndio itakuwa nafasi yao ya kujiuliza mbele ya FC Bayern Munich, kwani katika mechi 10 zilizopita dhidi ya timu hizo Bayern wameshinda mara tano, kapoteza mara mbili na sare mara tatu, mara ya mwisho Dortmund kuifunga Bayern ilikuwa April 26 2017 katika mchezo wa DFB Pokal uliyomalizika kwa magoli 2-3.
Kwa wapenzi wa Soka hapa nchini mchezo huu utakuwa live kupitia ST World Football ndani ya king’amuzi cha StarTimes ambao ndio warushaji pekee wa ligi hiyo yenye kasi zaidi barani Ulaya.
Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19