Leo November 14,2018 nakusogezea stori kutoka Mkoani Tabora ambapo inaelezwa kwamba Jeshi la Polisi Mkoani humo limelazimika kutumia mabomu kuwatawanya Wananchi waliokuwa wamekusanyika katika shule ya msingi ya Chemuchemu Mkoani humo wakidai kwamba Watoto wawili wanaosoma darasa la kwanza katika shule hiyo wametekwa na Watu waliokuwa na gari aina ya NOAH nyeusi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Tabora Kamishna Msaidizi Emmanuel Nley amesema kwamba bado wanafuatilia madai hayo ingawa mpaka sasa hawajapokea taarifa yeyote rasmi kuhusu kupotea kwa Watoto hao.
Aidha Kamanda ameongeza kuwa katika harakati za kuwatawanya Wananchi kwa kutumia mabomu hakuna Mtu yeyote aliyejeruhiwa wala mali zilizoharibiwa na Wananchi kwa sasa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.
Kamanda pia amewataka Wazazi kufika katika kituo cha Polisi kuripoti kama Watoto wao wamepotea.