Ifahamu hii kutokea Marekani ambapo Rapper Young Thug ameachiwa huru kutoka jela na hii ni baada ya kesi yake kusikilizwa mapema leo November 15,2018 na ameiomba radhi Mahakama kwa makosa aliyoyatenda.
Rapper huyo alikamatwa wiki iliyopitwa mjini Georgia na kurudishwa jela ikiwa kosa lake ni kwenda kinyume na masharti ya dhamana na kushindwa kuwasilisha vipimo vya afya wakati alipokuwa chini ya uangalizi (Probation).
Rapper Young Thug bado anakabiliwa na mashtaka mengine 8 ya jinai ikiwemo kukutwa na dawa za kulevya pamoja na silaha mwezi September,2017, inaelezwa kuwa rapper huyo anahitajika kuhudhuria ushauri na saa juu ya matumizi ya dawa za kulevya na kuwasilisha vipimo vya dawa za kulevya Mahakamani kila baada ya wiki mbili.
“Samahani kwa kutoitii Mahakama , samahani kwa kutomtii Muendesha Mashataka na kuwepo hapa kwa mara nyingine tena, nataka kwenda nyumbani nikaonane na familia yangu na kufanya vitu vilivyosahihi”
Rapper Young Thug amejutia makosa yake mbele ya Mahakama na wakili wake kusema kuwa tayari amejiadhibu mwenyewe kwa kutokula chakula kwa siku mbili tokea ameingia jela wiki iliyopita.
https://youtu.be/9_xKjyZXyes
“Yule Mtoto alikua akila nyama mbichi kwenye friji”