Kampuni ya Star Media kupitia chapa yake ya StarTimes wametangaza ujio wa Promosheni ya LIPA TUKUBUSTI katika msimu huu wa Siku Kuu. Promosheni hiyo imezinduliwa Alhamisi ya wiki hii kwatika Ukumbi wa Terrace, Slipway Masaki jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na waigizaji wa Bongo Movie pamoja na wasanii wa Muziki wa kizazi Kipya.
Katika Promosheni ya LIPA TUKUBUSTI wateja wa StarTimes watakuwa wakipatiwa vifurushi vikubwa zaidi kila watakapolipia na kujiunga na vifurushi vyao vya kawaida kwa malipo ya mwezi Mzima. Hali kadhalika kwa wateja wapya watapatiwa Antena BUREE kila watakaponunua king’amuzi cha Antenna kwenye maduka na mawakala wa StarTimes.
“Ving’amuzi vyetu, pata Antena ya BURE ukinunua king’amuzi cha Ante
Sio hivyo tu bali kupitia promosheni ya LIPA TUKUBUSTI wateja watanufaika kwa Kupata DISH la BUREEE kila watakaponunua luninga za Kidigitali za StarTimes za ukubwa wowote ule kuanzia Inchi 24, 32, 43 hadi ile Luninga Smati ya Inchi 55.
Kwa upande wa maudhui, Msimu huu wa Siku Kuu StarTimes wamejipanga vilivyo kwani wanaleta Filamu Mpya kabisa za Bongo Movie zilizosheheni mastaa wakali, Huku shindano la Bongo Star Search likiendelea, na kufikia hatua ya mchujo ndani ya Studio, Shindano hilo linaendelea kuonekana Kila siku saa tatu Usiku kupitia chaneli ya StarTimes Swahili Pekee.
“Tuna furaha kubwa kuwaletea filamu za Bongo Movie Mpya kabisa kwa mwezi mzima wa Disemba, filamu ambazo zina mastaa tunawaowapenda na kuwafatilia kila siku”>>> Zamaradi Nzowa
“Ni wakati wa kutengeneza kumbukukumbu nzuri na wale tuwapendao na StarTimes inalifanikisha hilo. Sio hayo tu bali tunaleta Msimu mpya wa Coppa Italia kwa mara ya kwanza kupitia StarTimes pekee, utamshuhudia Cristiano Ronaldo na Juventus kuanzia Disemba 5 kupitia chaneli zetu za Michezo”>>>>Zamaradi Nzowa
StarTimes ni kampuni ya Matangazo ya kidigitali inayoongoza Africa, ikihudumia zaidi ya wateja milioni 10 katika bara zima. StarTimes inamiliki jukwaa la maudhui lenye chaneli zaidi ya 480 zikiwemo chaneli za Habari, filamu, tamthiliya, michezo, burudani, vipindi vya watoto, mitindo, dini na vingine vingi.