Rapper Tekashi amerudi tena kwenye mikono ya mahakama baada ya kukamatwa Jumatatu ya November 17,2018 na kikosi cha FBI huku akishtakiwa kuwa na makosa 17 ya uhalifu kwa mujibu wa polisi na endapo atakutwa na hatia basi atahukumiwa kifungo cha miaka 30 au hadi kifungo cha maisha.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa idara ya ulinzi na usalama Marekani Tekashi amekutwa na makosa 17 ikiwemo kujihusisha na uhalifu na kikundi cha Nine Tery Bloods ambapo walifanya uvamizi wa silaha April 3,2018 akiwa na manager wake pamoja na members wengine wawili wa kundi hilo, Tekashi amekutwa na kosa la kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya.
Tekashi alikuwa kwenye kifungo cha nje(Probation) ya mwaka 1-4 kwa kosa lake la kumtumia kingono msichana mwenye umri mdogo mwaka 2015 na hata hivyo jaji amesema kuwa rapper huyo ni mtu hatari na hafai kuwa kwenye jamii hii ni baada ya Mwanasheria wa Tekashi kuiomba Mahakama impatie dhamana kwa sharti la kuchukua hati ya kusafiri na kulipa faini ya zaidi Billioni 2 za Kitanzania.
SEGEREA: Majizzo akumbuka mengi kuhusu ‘LULU’