Unaambiwa kusinzia mchana kwa zaidi ya saa moja ni dalili ya kisukari kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Wataalamu wa Japan ukitajwa kuwa wa kwanza na wa aina yake.
Watalaamu hao walipitia tafiti 21 zinazohusisha kiasi cha usingizi na uwezekano wa kupata magonjwa yasiyo ya kuambukiza, kisukari, shinikizo la damu, magonjwa ya moyo na kupooza ambazo zilihusisha watu 307,237 kutoka bara la Asia na nchi za magharibi.
Watafiti hao waligundua kuwa kusinzia mchana kwa muda unaozidi dakika 60 kunaongeza hatari ya kupata kisukari aina ya pili kwa asilimia 45 tofauti na kusinzia kusikozidi dakika 40.
Uchambuzi wa taarifa walizokuwa nazo Wataalamu hao ulidhihirisha kwamba hakuna hatari yoyote kwa Mtu anaesinzia mchana kwa dakika 40 lakini hatari huongezeka baada ya kuzidi dakika 60
Zipo sababu nyingi zinazoweza kuchangia hatari hiyo ambapo wanasisitiza usingizi mrefu wa mchana unaweza kumaanisha kuwa Mtu hakulala vizuri usiku suala linalohusishwa na msongo wa mawazo ambao ni chanzo cha kisukari.
Akitoa maoni juu ya majibu ya utafiti huo, Profesa Naveed Sattar ambae ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya metaboliki kutoka Chuo Kikuu cha Glasgow, Uingereza anasema “Utafiti huu unaonyesha uhusiano wa kisukari na usingizi mrefu wa mchana, inawezekana kinachosababisha kisukari ndio kinacholeta usingizi huo, inawezekana ni sukari imezidi mwilini hivyo usingizi mrefu kuwa dalili ya kisukari.”
NYOTA 3: MAISHA YA HASSAN NGARENARO, RAFIKI ZAKE 18 WAMEUWAWA KWA WIZI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA
VIDEO: MUME KAENDA KAZINI, WIFE KALETA MCHEPUKO NYUMBANI…. BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA