Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linamshikilia Kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Hassan Abdallah Athuman, umri miaka 38 kwa tuhuma za kujifanya Daktari wa magonjwa ya binadamu bila kuwa na vibali maalum.
Kamanda wa Polisi mkoani humo Gilles Muroto amezungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake leo November 24, 2018.
RPC Muroto “Huyu tumemkamata eneo la Kijiji cha Mwakisabe alikuwa akitoa Taaluma ya Utabibu bila ya kusomea ni Daktari feki, huyu aliwahi kukamatwa huko nyuma kwa kosa kama hili, alitorka Mahakamani”
TAARIFA: FIESTA 2018 DSM ILIYOKUA IFANYIKE LEO IMEAHIRISHWA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUPATA TAARIFA HII