Kupitia mahojiano aliyoyafanya rapper Meek Mill na mtandao wa Vulture amegusia kufanya collabo na rapper Drake ambaye wamekuwa kwenye bifu kwa muda mrefu na kumaliza tofauti zao September,2018.
Rapper Meek Mill ambaye yupo mbioni kuachia album yake mpya ya “Championships” siku ya November 30,2018 amegusia pia ishu ya kuwasiliana na Drake tokea mwaka jana kabla ya kwenda jela na kusema kuwa bifu lao halikuleta madhara yoyote na kutokana na kipindi hicho amekuwa mwenye nguvu.
Meek Mill >>>“Mimi na Drake tumekuwa tukiwasiliana tokea mwaka jana kabla ya kwenda jela, hakukuwa na kitu cha maana kilichokuwa kikiendelea zaidi ya bidu kwenye rap na hatukuleta madhara yoyote kati yetu, nahisi ilitufanya tupitie changamoto tu tofauti kwangu na kwenye kazi, ilinifanya niwe imara zaidi “
EXCLUSIVE: Lord Eyes kafunguka kuwa mapenzini na Wolper “Namkubali, Baby Mama wangu yupo..”